Wakuu wa Upelelezi wakutana na IGP Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka wakuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kuendelea Kuimarisha usalama, amani na utulivu kwa raia na mali miongoni mwa nchi washirika kutokana na malengo tuliyojiwekea hasa ushirikiano kwenye mafunzo na ubadilishanaji wa taarifa.

IGP Sirro amesema hayo wakati akifungua mkutano wa Wakuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa Nchi za Mashariki Mwa Afrika utakaofanyika kwa muda wa siku mbili Jijini Arusha mkutano ambao utafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 21 wa Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika.

Aidha, ameainisha kuwa, kukutana kwa wakuu hao wa Upelelezi kutaibua chachu pamoja na mikakati thabiti ya kukabiliana na uhalifu wa makosa yanayovuka mipaka na uhalifu wa kupanga.

Kwa upande wake Mkuu wa Sekretarieti ya Ofisi za kanda Nairob Gedion Kimilu, amesema kuwa, uhalifu wa kimataifa sasa umeamia kwenye mifumo ya kitekinolojia kutokana na kukua kwa utandawazi hivyo nchi wanachama wa EAPCCO ni lazima kujidhatiti katika kuzuia uhalifu kwa njia ya kimtandao

Naye Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Boaz amesema kuwa, maazimio ya mkutano huu yatakuwa sehemu ya agenda za mkutano mkuu wa 21 ili yaweze kujadiliwa kwa pamoja ikiwemo masuala ya matishio ya kigaidi hususan kwa nchi wanachama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad