Waliojiunganishia bomba la mafuta waachiwa huru


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka na kuwaachia huru watuhumiwa watano waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta la Mamlaka ya Bandari (TPA) eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.


Uamuzi huo umetolewa leo, Septemba 23, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya Wakili wa Serikali, Simon Wankyo, kuieleza Mahakama kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.



Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba,  ameeleza kuwa kwa vile DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo, watuhumiwa hao anawaachia huru. Baada ya kuachiwa huru watuhumiwa hao walielekea chumba cha askari polisi kwa ajili ya taratibu za kusaini ili waweze kuondoka na baada ya kutimiza hayo waliondoka huku ndugu zao wakiwakumbatia kwa nyuso za furaha kuwaona ndugu zao wakiwa huru.



Walioachiwa huru na mahakama hiyo ni Audai Ismail (43) mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban Kamwa na Zubery Ally.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad