Wanafunzi 7 wafariki baada kuangukiwa na jengo la darasa Kenya


Wanafunzi saba wamethibitishwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya darasa la shule yao kuporomoka leo  Jumatatu  Septemba 23, 2019 asubuhi Nairobi nchini Kenya.

Jengo la mbao la shule ya msingi ya Precious Talent liliporomoka muda mfupi kabla ya masomo ya siku kuanza.

Wanafunzi kadhaa bado wamekwama ndani ya jengo hilo na shughuli za uokozi zinaendelea.

Mafisa wa zima moto wa Baraza la jiji la Nairobi kwa ushirikiano na Shirika la Msalaba mwekundu wanasaidiana na wenyeji kuwaokua watoto waliokwama chini ya jengo hilo.

Kamanda wa polisi George Seda na mbunge wa eneo la Dagoreti, John Kiarie, wamethibitisha kuongezeka kwa idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo.

Mkurungezi wa shule hiyo ya kibinafsi, Moses Wainaina Ndirangu, amaeiambia Runinga ya Citizen nchini Kenya kuwa jengo hilo liliathiriwa na ujenzi wa bomba la maji taka karibu unaoendelea karibu na hapo.

Baadhi ya wanafunzi wanasemekana kukiimbilia makaazi ya watu walio karibu na mtaa waDagoretti, Magharibi mwa Jiji la Nairobi baada ya jengo la shule kuporomoka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad