Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Kanyasu Constatine amewahakikishia wasanii wote nchini kuwa katika kipindi chake cha Uongozi ataondoa vikwazo vyote vilivyokuwa vinapelekea wasitumie madhari ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini wakati wa kutengeneza kazi zao Sanaa.
Pia, Amewataka wasanii na watu maarufu wapende vitu vya kwao badala ya kuona ufahali wa kuitumia madhari za nchi nje ilhali Tanzania imejali kuwa kuwa utajiri wa mandhari za kipekee na zenye mvuto wa hali ya juu.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam kwenye hafla iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na na vijana wa Tanzania Vision 2025 kwa kuwaalika watu maarufu hususan Wasanii kwenye chakula cha jioni, Naibu Waziri Kanyasu amewataka wasanii hao watumie kalama na ushawishi walio nao katika kuhamasisha utalii wa ndani.
Amewataka wasanii hao wasijione kuwa wao ni watu Wanyonge badala yake wajiamini kwa vile ni watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii kupitia kazi zao za Sanaa.