Baadhi ya wananchi wa Burega katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wamevamia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakiwa na mwili wa mtoto mchanga kwa lengo la kufikisha malalamiko yao katika Ofisi za Manispaa kufuatia kuzuiwa kumzika kichanga huyo na mtu aliyedaiwa kufukia kaburi akipinga kutumika kwa eneo lake.
Wananchi hao wamesema wamechoshwa na hali hiyo inayojirudia inayofanywa na mtu huyo anayedai anazo nyaraka zote huku eneo hilo likifahamika kuwa ni la makaburi.
Hata hivyo baada ya mzozo huo, Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Idara ya Ardhi ya Manispaa na Mkurugenzi Mailwa Pangani wamewaruhusu wananchi hao kuzika kichanga hicho kwenye eneo hilo kwa maelezo kuwa ni la maziko na sasa wanamtafuta mhusika ili sheria ichukue mkondo wake.
Wavamia Ofisi za Manispaa baada ya kuzuiwa kumzika mtoto mchanga
0
September 25, 2019
Tags