Waziri Lugola: Sijawahi kupokea rufaa ya kulalamika kunyimwa kufanya mikutano, Wanakurupuka


Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania,  Kangi Lugola amesema wanaolalamika na kuanza kufanya maandamano na mikutano wanavyotaka wao bila kibali ni  lazima wakutane na mkono wa sheria kwani polisi iko imara na hawawezi kuachwa.

amesema Lugola alisema sheria zikifuatwa hakuna  shida itakayotokea lakini kinyume na hapo mambo yanakuwa tofauti.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo jana baada ya kuzindua ofisi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mjini Dodoma.

Alisema sheria inawataka watu wanaotaka kukusanyika kulipa taarifa Jeshi la Polisi, wakiona kimya wanaendelea ila wakipewa barua ya zuio wanatakiwa kusitisha shughuli hizo na kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo.

amesema hajawahi kupokea barua yoyote kutoka chama cha siasa kulalamika kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara au maandamano.

“Tangu nimeteuliwa sijawahi kupokea hata rufaa kulalamika kuwa wamenyimwa haki badala yake wanakurupuka na kulalamika sasa mimi nifanyeje,” amesema Lugola

“Tunao polisi imara, hakuna polisi anayeweza kuwakimbia watu hata kidogo lazima wasonge mbele, sasa hapo ndio mtasikia huyu kaumia au kaumizwa yote ni kwa sababu hawafuati sheria,” alisema Lugola.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad