Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene, ametoa siku 14 kwa watengenezaji na wasambazaji wa mifuko mbadala hapa nchini kuhakikisha mifuko hiyo inakidhi vigezo vyote stahiki ikiwamo uwekaji wa nembo ya mmiliki au kampuni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara Bandari ya Dar es Salaam, Simbachawene alisema uwapo wa wazalishaji wa mifuko mbadala ambao hawakidhi vigezo na masharti yaliyoweka na mamlaka husika inasababisha wazalishaji wa ndani kukosa soko na kupoteza mapato la serikali.
“Ni lazima tujue nani anazalisha na kusambaza mifuko hii mbadala, hawa wanaozalisha ndani na kufuata taratibu zote wanakosa soko kwa sababu ya wengine wanaofanya biashara hii kiholela bila kufuata taratibu.” alisema Waziri Simbachawene.
Mbali ya agizo hilo, alisema baada ya muda kufika msako mkali utafanyika na kwa yeyote atakayekutwa akizalisha au kuuza mifuko mbadala isiyofikia na vigezo vilivyowekwa na mamlaka husika, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwamo pia kuchomwa kwa mifuko hiyo.
Waziri Simbachawene ataka mifuko mbadala kuwekwa nembo
0
September 26, 2019
Tags