Yanga Yaandaliwa Mapokezi Mazito Zambia


KIKOSI cha Yanga kimeondoka Jana Jumanne kuelekea nchini Zambia tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco United ambapo Watanzania waishio nchini humo wamejipanga kuhakikisha wanaipa sapoti timu hiyo.



Yanga itarudiana na Zesco United siku ya Jumamosi mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, katika mechi ya kwanza iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.



Yanga inahitaji ushindi wa aina yoyote ili iweze kufanikiwa kusonga mbele katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.



Akizungumza na Championi Jumatano, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Rogers Gumbo alisema kuwa, kamati yake imejiandaa vyema kuhakikisha wanashinda mchezo huo ambapo kikosi kitaweka kambi ya siku moja Lusaka kisha kitaendelea na safari na kudai kuwa Watanzania waishio huko wameonyesha kuhamasika kwa kuipa sapoti timu yao.



“Hamasa ipo kubwa timu inaondoka kesho (jana) kuelekea Zambia na itafi kia Lusaka, itakaa siku moja kisha Alhamisi kikosi kitaondoka kuelekea Ndola tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu.



“Kamati yetu imekutana na wachezaji katika kuwapa hamasa kuhakikisha wanafanikiwa kushinda mchezo huo ili kuingia hatua ya makundi ambayo ndiyo tageti yetu.



“Watanzania waishio Zambia wameonyesha ushirikiano wa hali ya juu kuelekea mchezo huo kutokana na sapoti yao, hivyo tuna imani tutapata matokeo mazuri,” alisema Gumbo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad