Yanga Yagomea Tena Nembo Nyekundu ya Mdhamini



KLABU ya Yanga imewaonya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kamwe isithubutu kuwalazimisha kuvaa jezi yenye nembo nyekundu ya mdhamini .
Hivi karibuni TFF iliingia mkataba na Kampuni ya simu ya Vodacom kudhamini Ligi Kuu Bara kwa udhamini wenye thamani ya Sh 9 bilioni.

Kampuni ya Vodacom inatumia nembo nyekundu kama utambulisho wao ambapo Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wanasikia tu kuwa msimu huu lazima kila timu ivae jezi yenye nembo nyekundu lakini wao hawatakubali hilo.
"Tumesikia maneno mengi  kuwa msimu huu lazima kila timu ivae jezi yenye nembo nyekundu ambayo ni ya mdhamini lakini hilo kwetu hatutakubali.

"Katiba ya Yanga ambayo imepitishwa na  TFF, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Msajili inatambua rangi tatu za Klabu, njano, kijani na nyeusi, hivyo hiyo rangi nyekundu hatuitambui"alisema Mwakalebela.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad