Zidane ambebesha majukumu Hazard kuiuwa PSG leo,

Tangu atimke Chelsea na kujiunga na miamba ya soka nchini Hispania ndani ya klabu ya Real Madrid kwa dau lililoripotiwa la pauni milioni 130, Eden Hazard muda mwingi amekuwa akiuguza majeraha yake.

Kwa mara ya kwanza mwishoni mwa juma lililopita Hazard ameweza kucheza mchezo wake wa kwanza kwa Los Blancos hao wakati akitokea benchi na Real Madrid kuchomoza na ushindi wa mabao 3 – 2 dhidi ya Levante.

Mara baada ya nyota huyo kuonyesha kuanza kuwa fiti kocha wake, Zinedine Zidane sasa anafikiria kumbebesha majukumu kwenye mchezo wa usiku wa leo Champions League dhidi ya matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain.

”Kama unavyojua siku zote nimekuwa nikifikiria Hazard anaweza kubeba jukumu la Madrid, anaweza kuleta mabadiliko na ukweli ni kwamba anaweza kuonyesha hilo Real Madrid.

Zinedine Zidane ameongeza “Sitaki kumlinganisha, lakini nafikiria kwamba atakuwa mchezaji muhimu sana hapo baadae ndani ya Real Madrid.”

Real Madrid news: Eden Hazard

Kwa sasa Real inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya Hispania, La Liga kwa tofauto ya pointi mbili na vinara Sevilla wenye alama 10.

“Tunatarajia kushuhudia makubwa kati ya PSG na Real Madrid, lakini ndiyo tunaanza msimu tunaweza kufanya vizuri zaidi,” Zidane.

”Ni lazima tuwe bora na kufanya hivyo kwa uwezo wetu wote lakini nafikiria itakuwa hivyo hata na kwa PSG. Sifahamu hasa mapungufu ya PSG lakini nafikiria kwamba timu yao imezidi kuimarika ni klabu kubwa lakini kushinda taji la Champions League siyo kitu rahisi.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad