Zijue Athari za kubaki Kwenye Penzi lililoisha


Katika mahusiano kitu kikubwa kinachozungumziwa ni hisia na mahusiano ni uwekezaji na ukiwekeza mahali na uone haupati faida wala marejesho yoyote, ni lazima utaona imekuwa kama biashara kichaa.


Kwa Mwanamke na Mwanaume kila mmoja anatarajia marejesho kutoka kwa mwingine, ikiwemo kupatiwa huduma ama kujuliwa hali lakini unakuja kushangaa kila kitu kinakuja kuwa tofatuti.

Mwanasaikolojia John Ambrose anasema kuwa kuna aina takribani tano za mahusiano, katika mahusiano hayo kuna watu ambao wanayo mahaba yaliyopitiliza, kuna wengine hawapendi kuwajibika wengi wao wakiwa wanaume kwa maana nyingine ni watu wenye dharau, Ambrose anasema ukiolewa na mtu wa aina hii lazima utaumia.

Mahusiano pia  yanategemea haiba ya mtu, kuna watu ni wapole na wanyenyekevu na hawapendi mahusiano yao yaharibike, lakini pia kuna watu wengine ambao wameathiriwa na malezi ambao hawezi kufanya maamuzi bila familia zao .

Lakini hisia ni kama 'keyboard' inayotawala mahusiano na inategemea hisia za mtu zimejengeka vipi kimazingira. Wanawake wapole na wanyenyekevu wasiopenda changamoto ndio viumbe wanaoumia zaidi katika mahusiano.

Mwanasaikolojia huyu ameitaja jinsia ya Kike ndiyo rahisi sana kubaki katika penzi lililoisha na hii inaenda zaidi kwa wanawake walio katika ndoa, ambao mara nyingi hubaki kwa kuhofia maisha ya watoto wao waliowazaa kwa kuhofia endapo akiondoka watoto hao watateseka.

Mwanasaikolojia huyo wa masuala ya mahusiano, amezitaja athari za kubaki katika mahusiano yaliyokwisha ni pamoja na vifo na watu kuuana, kuingia kwenye mahusiano ya kulazimisha.

Jambo lingine ni kuingia katika mahusiano ambayo hatujayafanyia utafiti, hali inayopelekea watu kupata  makovu ya Moyo, ugonjwa wa upweke na kupelekea kinga ya mwili kushuka na kukutwa na mafua ya mara kwa mara.

Athari nyingine ni ya uchumi na kupata Sonona kwa kushindwa kufanya shughuli zako na utendaji wa kazi kushuka na kuwa na hofu kubwa huku wengine wakiamua kujiua na kuwa wakatili .

Aidha Ambrose anatoa ushauri kwa watu ambao bado hawako katika mahusiano, kwamba mapenzi ni Sayansi hivyo ni vyema ukasoma kwanza kabla ya kuingia na malumbano yanayotokea yanatokana na jinsi ambavyo mlivyoanza na kwa upande wa watu waliokatika mahusiano anawashauri ni vyema kutunza mazuri ya mwenzako zaidi, kuliko kutunza mabaya yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad