Zitto na Lissu waipa nguvu ACT Wazalendo

Mshauri Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa, kuonekana pamoja kwa viongozi wawil vya vyama vya siasa vya upinzani, Zitto Kabwe (ACT) na Tundu Lissu (CHADEMA), kumewapa nguvu kuelekea uchaguzi wa 2020.



Maalim ameeleza kuwa wawili hao waliokutana nchini Ubelgiji ambako Tundu Lissu anaendelea na matibabu, wameonesha njia nzuri.

''Zitto Kabwe na Tundu Lissu wametupa faraja na kutuonesha njia kuelekea 2020. Nawapongeza na kuwatia moyo kutekeleza wajibu wa kihistoria kwa Tanzania wakati tunaelekea uchaguzi mkuu wa 2020 ambao ni uchaguzi muhimu kuliko chaguzi zote katika kuamua mustakabali wa Tanzania''.

Zitto Kabwe alirusha video mtandaoni ikionesha yupo na Tundu Lissu, wakitembea kwenye mitaa huko Ubelgiji huku wakisema mwanasheria huyo wa CHADEMA yupo tayari kurejea nchini.

Kwa mujibu wa ratiba aliyowahi kuitoa mwenyewe, Tundu Lissu atarejea nchini Septemba 7, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoondoka kwenda kutibiwa mwaka 2017, kutokana na kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mkoani Dodoma.




Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dodoma ni Jiji. Wote mnnakaribishwa.

    Mstafutie kiki Aliyekuwa mbunge Singida Mashriki naKukwaza mweyekiti wake...!!!

    Mkamharibia picha nzima Mgonjwa.

    Mweyewe aesha jiwekea Mazingira ya asylum Seekerkwa hiyo msijisemeshe kutafutauhonganishi kama alivyo fukuzwa Mtoto wa Uvira. Sijui lini atarudi kwao. Hivyo anaishi kata Gani?

    ReplyDelete
  2. Dodoma ni Jiji. Wote mnna karibishwa.

    Msimtafutie kiki Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki na Kumkwaza mweyekiti wake...!!!

    Mka muharibia picha nzima Mgonjwa.

    Mwenyewe amesha jiwekea Mazingira ya asylum Seeker kwa hiyo msijisemeshe kutafuta kumnchonganisha kama alivyo fukuzwa Mtoto wa Uvira. Sijui lini atarudi kwao. Hivyo anaishi kata Gani?

    Akijua fika kuwa Tanzania ni ya Watanzania na Wahamiaji Haramu tumeanza Kuwapekenyua.

    ReplyDelete
  3. Hivyo Ubeligiji iko wapi? Lubumbshi au Ruvuvu?

    Ratiba imesha bidilishwa mtatagaziwa mwishoni au katikati ya mwezi wa kumi
    sijui oktoba novemba febluali.

    MPaka majibu ya ukimbizi yakitoka kabla ya pasipoti za kieletoiki.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad