KIMENUKA..Chuo Kikuu Moi Chafungwa....Vurugu za Wanafunzi Usipime
0
October 13, 2019
Chuo kikuu cha Moi nchini Kenya, kimefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na vurugu za wanafunzi ambao walifikia hatua ya kupambana na polisi waliokuwa wakiwatuliza.
Maafisa wa ushirika wa wanafunzi chuoni hapo wamesema kuwa baada ya jaribio la kutaka kukutana na kuzungumza na viongozi wa chuo hicho siku ya jumatano kugonga mwamba hawakuwa na chaguo lingine zaidi ya kuandamana.
Kwamujibu wa mahitaji wanayohitaji wanafunzi hao ni 8 yakiwemo yakuomba kuajiriwa kwa wahidhiri zaidi, kupunguzwa kwa kiasi cha fedha cha kufanya mitihani ya kurudia (supplementary exams) na kufukuzwa kazi kwa mlinzi mkuu wa chuo hicho.
Lakini kutokana na vurugu za wanafunzi hao chuo hicho kimetoa notisi ya kuwataka wanafunzi kuondoka chuoni hapo mara moja hadi watakapo tangaziwa hatua zaidi.
Ikumbukwe kuwa kutokana na vurugu za wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kenya tayari vyuo vitatu vimefungwa kwa muda usiojulikana, chuo kikuu kenyatta kilifungwa jumatano na Masinde Muliro kilifungwa mwishoni mwa mwezi uliopita.
Tags