Adhabu ya Viboko ilijenga Taifa Lenye Nidhamu kuanzia Mashuleni Mpaka Majumbani !


Nakumbuka kipindi kile cha shule ya msingi tulikuwa na mwalimu anaitwa Mr Kitunga ukiambiwa unaenda kuoga fimbo zake mikojo inakutoka kabla ya kufika kwenye adhabu yenyewe na ukifika shule tayari watu wapo mstarini ni vyema urudi hospitali kwenda kuchukua cheti cha dokta uzuge unaumwa

Hali ile ilijenga nidhamu ya hali ya juu na kutochelewa shule na ndio watu waliitumia kujenga nidhamu na uwajibikaji mpaka makazini

Lakini kilipokuja hiki kizazi cha laktojeni na vyama vingi vya siasa kila kitu kimebadilika, taifa limekuwa na vijana wa hovyo wa kuvaa kata K. Hata ukimtuma mtoto wa jirani anakukatalia bila soni.

Toto halijawahi kupigwa hata kibao akiadhibiwa na mzazi wake basi ni kwa njiti ya chelewa,matokeo yake ndio hawa wanaona Rais John Magufuli kila alifanyalo anawaonea hawawezi kuwajibika wala hawana nidhamu wala uzalendo mwisho wa siku anafikia kuchoma shule moto.

Ni vyema sasa ifikiriwe kurudisha adhabu ya viboko ili watoto wanyooke tuondoe taifa legelege,nidhamu ichukue mkondo wake

Ni hatari siasa ikimeza kila jambo eti leo mwanasiasa anasimama na kutafuta kiki kisa mwanafunzi kaadhibiwa na mwalimu ambaye ni sawa na mlezi wake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad