Afrika Kusini imeipa shirika la ndege la kitaifa la Zimbabwe, idhini ya kusafiri katika mji wa Johannesburg. Haya yanajiri baada ya shirika hilo kupigwa marufuku ya kutotumia viwanja vya ndege nchini Afrika Kusini, kutokana na malimbikizi ya ada.
Juma lililopita, ndege ya inayomilikiwa na serikali ya Zimbabwe ilizuiwa kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Johannesburg baada ya kushindwa kulipia huduma za uwanja wa ndege.
Kwa mjibu wa usimamizi mkuu wa uwanja wa ndege wa Johannesburg, hali hii ilitatuliwa siku ya Ijumaa iliyopita, baada ya Zimbabwe kulipa deni lake lote.
Air Zimbabwe inapaswa kulipa ada ya kutumia viwanja vya ndege, kupakia ndege na huduma kwa wateja wake nchini Afrika kusini mara moja kwa wiki.