Amber Lulu Kadata Kweli..Aeleza Alivyoshea Mwanaume na Gigy

 
Kwa kawaida siku ya Jumatano watu wameipendekeza kuita 'Woman Crush Wednesday', ambapo leo tumepiga stori na Amber Lulu, ambaye amefunguka suala la kushea Mwanaume na Gigy Money pamoja na wanawake kupenda pesa.


Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, kuhusu kugombania mwanaume na Gigy Money, Amber Lulu amekiri kuwa alishawahi kushea mwanaume mmoja kipindi cha huko nyuma.

"Kutokana na 'Lifestyle' ya sasa hivi watu hawamjui bwana angu kwa hiyo wanajitahidi kumtafuta na kuotea kama natoka na nani, mimi sijawahi kugombana na mtu hizo stori za kugombania mwanaume ni zamani sana, kama miaka mitatu au miwili nyuma huko , nakumbuka mwanaume ambaye mimi nilipita na yeye alipita ni Casto Dickson'' amesema Amber Lulu.

Aidha msanii huyo amezungumzia suala la wanawake kudanga ili wapate pesa, ambapo amesema kuwa.

"Inatokeaga mara nyingi sana, Bongo hakuna mwanamke awe na mtu halafu akatae pesa, kila mtu anategemea mwanaume mwenye pesa, halafu sisi wanawake tunapenda kupewa ila inategemea unadanga kiasi gani" amesema Amber Lulu

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu ni ukosefu wa Maadili. na msitowe katika blog yetu hiii. Mkuu wa nchi analipinga jambo hili juu ya wanafunzi kwa nguvu zake zote.

    ReplyDelete
  2. Huu ni ukosefu wa Maadili. na msitowe katika blog yetu hiii. Mkuu wa nchi analipinga jambo hili juu ya wanafunzi kwa nguvu zake zote.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad