Askofu wa kanisa wa Mlima wa moto Bi Getrude Rwakatare, atoa maana ya “Upepo wa Kisulisuli”
0
October 18, 2019
Askofu wa kanisa wa Mlima wa moto Bi Getrude Rwakatare, ametoa maelezo kuhusu video fupi ya maombi yake ya upepo wa kisulisuli ambayo inazunguka zaidi katika mitandao ya kijamii na mitaani.
Kwa mujibu wa EATV: Bi Getrude Rwakatare amesema hakuamini kama maombi yake ya upepo wa kisulisuli yataenea zaidi kwa watu na kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa kweli namshukuru Mungu kupitia ile video fupi inavyosambaa, kufika mbali na kupokelewa vizuri na katika jamii na kugusa mioyo za watu, Upepo wa kisulisuli ni upepo wa kimbunga ambao unakuja ghafla na inabeba chochote ambacho kipo njiani na huvutwa kutoka Magharibi na Mashariki hadi Kaskazini na Kusini, kwahiyo upepo huu ni nguvu na miujiza ya Mungu” amesema Bi Getrude Rwakatare.
Pia amesema nia ya kufanya hivyo ni kuwasaidia Wanawake ambao hawajaingia kwenye ndoa, wapate Wanaume wa kuwaoa maana dunia hii Wanawake wamekuwa wengi ila hawapati bahati ya kuolewa na kubaki kuhangaika kwa waganga na kutumia dawa. ameongeza.
Aidha amesema maombi haya ya upepo wa kisulisuli yataendelea Jumapili hii kama kuna mtu atakuwa na tatizo lake anaweza akaenda kwenye Ibada kanisani Mlima wa moto na itaenda hadi mikoani sio kwa wakazi wa Dar Es Salaam tu.
Tags