BAKITA watoa kauli kuhusu ‘Upepo wa kisulisuli’ wa mchungaji Rwakatale


Kwa siku mbili sasa kumekuwa na video za mchungaji wa kanisa la Mlima wa Moto, Dkt. Gertrude Rwakatale akiwaombea waumini wake wa kike wapate wanaume wa kuwaoa huku akitamka neno ‘Upepo wa Kisuli suli’ jambo ambalo kila mtu amekuwa na tafsiri tofauti tofauti ya maana halisi ya upepo huo.


Kufuatia tafsiri hizo, Msanifu wa Lugha Mkuu kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Consolata Mushi, ameeleza maana halisi ya neno hilo ukiachana na ile ya kiimani, kupitia Kamusi sanifu ya Kiswahili Fasaha.

Bi. Consolata amesema ”Muktadha wa neno kisulisuli nikiangalia ni kwenye masuala ya imani, kumbukeni masuala ya imani kwao ni kusadiki jambo ambalo, hujaliona na kuliamini kwamba litatokana kama lilivyo kwa mujibu wa msamiati wa Kiswahili, neno Kisulisuli lina maana ya upepo unosafiri na kuzunguka na kwenda kwa kasi au kwa haraka”.

Kuhusu kauli ya Mama Rwakatare, Bi. Consolata  amesema neno hilo katika muktadha wake na alimaanisha kwamba ni jambo ambalo litatokea kama kimbunga kwa sababu upepo wa aina hiyo hutokea ghafla.

“Kama yeye alitumia kama mchumba anaweza akaja kama upepo wa kisulisuli ni muktadha wa imani, kwamba wapo na watajitokeza bila kutarajia, sasa msije mkaiingiza kwamba atajitokeza anazunguka kama upepo Laa! hasha! muktadha uongozwe kwenye kupata maana ya maneno, kwamba umekwenda kanisani ni msichana ama mvulana bila mwenzio lakini pale baada ya sala na imani akatokea mwenzio hukutarajia, hukupanga,” amesema Bi. Consolata.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad