Balinya: Yanga Bado ni ya Kimataifa

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mganda, Juma Balinya, ni kama ametupa dongo kwa mashabiki wa Simba baada ya kufunguka kuwa wao bado wapo katika mashindano ya Afrika, licha ya kupoteza mbele ya Zesco kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumamosi iliyopita.



Zesco United, juzi Jumamosi walikatisha safari ya Yanga ya kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa hapa nchini.

Yanga baada ya kufungwa juzi, sasa wanaangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kucheza mechi za mtoano kusaka nafasi ya kutinga makundi.



Droo ya hatua hiyo inatarajiwa kufanyika Oktoba 9 na hapo ndipo Yanga itajua inacheza dhidi ya timu gani.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Balinya alisema anawashangaa watu wanaowacheka kufungwa na Zesco na kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa kwani wao hawajapoteza kitu kwa kuwa bado wanayo nafasi ya kutinga katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.



“Sisi hakuna tulichopoteza kwenye mashindano ya Afrika, tumeshuka daraja moja chini na sasa tunashiriki Kombe la Shirikisho, hivyo bado tupo na hatujakata tamaa, tutafanya kila kitu kuhakikisha tunamfunga kila atakayekuja mbele yetu,” alisema Balinya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad