Bao la Makame Lazua Gumzo Mitandaoni

Bao alilofunga kiungo fundi wa Yanga kutoka Zanzibar katika mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union ya Tanga limezidi kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na likileta sintofahamu kama lilikuwa halali au la.

Katika mchezo huo, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa kwanza katika msimu huu wa ligi tangu uanze baada ya mechi mbili za mwanzo kuambulia alama moja.

Bao hilo la Makame lililoipa ushindi Yanga wa 1-0 dhidi ya wagosi hao wa kaya limekuwa likizungumziwa zaidi, wengi wameonekana wakieleza lilivuka msitari wa kati na wengine wamesema hapana.

Baadhi ya wadau pia wamefunguka kuwa yawezekana Mwamuzi wa kati hakuona vizuri kutokana na umbali baina yake na Makame alipokuwa pia kuona vizuri mstari wa langoni kama mpira ulikuwa umevuka au haujavuka.

Licha ya Mwamuzi kuruhusu, Mwamuzi wa pembeni alinyoosha kibendera juu kuashiria kuwa si bao lakini hakukuwa na mawasiliano mazuri kw apande mbili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad