Basi la Abood Lapata Ajali Dar


BASI la abiria mali ya Kampuni ya Abood Bus Services Ltd, limepata ajali mbaya maeneo ya Kimara Temboji jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo, Jumatano, Oktoba 30, 2019.



Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanadai kuwa, basi hilo lilikuwa likitoka Stendi ya Mabasi, Ubungo Dar, kupitia Barabara ya Morogoro, baada ya dereva wa basi hilo kugonga gema, lilipolekea taili la basi hilo kupinda na kwamba hakuna abiria yeyote alijeruhiwa.



Akizungumza leo Oktoba 30, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 2:00 asubuhi, huku chanzo akikitaja kuwa ni wembamba wa barabara hiyo ambayo kwa sasa ipo katika upanuzi.



“Ni kweli kuna taarifa hizo kwamba, limeacha barabara katika barabara zetu hizi zinazofanyiwa matengenezo ya kupanuliwa, Basi limeinama na sio kama limepinduka na hakuna aliyeumia, njia ni nyembamba na hii njia kuna vigema vingi, kwahiyo Dereva katika kuingia, aliingia vibaya na tairi likalala na kupelekea Basi likainama” amesema Kamanda Taibu.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad