Basi la Kanisa Lakamatwa Likisafirisha Misokoto ya Bangi



Polisi waliokuwa wakifanya Doria kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa Oktoba 15, wamekamata basi la Kanisa la PEFA likiwa na Misokoto 230 ya bangi iliyokuwa imesundwa kwenye eneo la mizigo

Kulingana na ripoti ya Polisi, basi hilo lilikuwa limesafirisha waombolezaji kutoka Kilifi kwenda Homa Bay na wakati wa kurudi likapakiwa na bangi hiyo

Tayari dereva wa basi hilo pamoja na watu wengine wawili wametiwa mbaroni ili kusaidia Polisi kwenye uchunguzi wa kisa hicho

Bangi hiyo inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 1  

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad