Mkuu wa Takwimu za bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Khamis Abdul-rahman Msham amesema mfumko wa bei wa mwaka umeongezeka kwa 2.2 mwezi wa Septemba 2019, ukilinganisha na mwezi uliopita wa August 2019 ambapo ulikuwa 2.1.
Ameyaeleza hayo huko katika Ofisi za Mtakwimu ulioko huko Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ongezeko wa mfumko wa bei .
Amesema Kushuka kwa baadhi ya bidhaa muhimu nchini kupelekea kushuka kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 0.8 kwa mwezi wa Agosti kulinganisha na asilimia 1.2 kwa mwezi wa Septemba .
Pia amefahamisha kuwa upande wa bidhaa hizo ikiwemo samaki ameshuka kwa asilimia 3.1 tan rice 2,5 ndizi za mtwike 4.7 mchele wa Mbeya 1.9 na sukari 0.3.
Nae Mhadhiri wa uchumi kutoka chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA, Dkt. Suleiman Msaraka amefahamisha kuwa mabadiliko ya faharisi za bei yanaendana na wakati uliopo kwa kulinganisha na
mwezi kwani bado tupo katika hali nzuri kama ilivyakadiriwa na Serikali .
Kwa Upande wa Meneja wa Uchumi Benki kuu ya Tanzania Tawi la Zanzibar Moto Ngwinganele Lugobi amesema mfumko umeongezeka ila sio sana na kwa upande wa soko la Zanzibar liko vizuri.