Waliokufa ni miongoni mwa watu sita walioshikana mikono na kusimama katika kina cha maji marefu karibu na bwawa la Pambar kabla ya mmoja wao kuteleza, na kujaribu kumuokoa mwengine. Mume wa mwanamke huyo aliweza kumuokoa dadake lakini wengine wakafa maji. India ina idadi kubwa ya watu wanaofariki kutokana na vifo vya selfie.
India iliripoti vifo vya watu 259 kati ya 2011 na 2017 kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la maabara ya tiba nchini Marekani; na katika janga hili inafuatiwa na Urusi, Marekani na Pakistan.
Wanandoa hao kutoka Bargur katika eneo la Krishnagiri, walikuwa wakitembelea familia huko Uthangarai..
Dada huyo alivutwa na nduguye lakini wengine wanne wakapotea ndani ya maji. Maafisa wa polisi wanasema kwamba miili yao baadaye ilipatikana na uchunguzi kufanywa. Ni kisa cha hivi karibuni miongoni mwa msururu wa vile vya kupiga selfie nchini India. Wataalam walionya kwamba watu wanafanya hatari ili kuwafurahisha watu wa familia zao katika mitandao ya kijamii.
Katika jimbo la Haryana mnamo mwezi Mei , vijana watatu waliokuwa wakipiga picha za selfie katika reli waliruka kutoka katika njia ya barabara hiyo ya treni walipoona gari hilo likikaribia walikokuwa, kabla ya kuuawa na treni nyengie iliokuwa inajiri kutoka upande mwengine wa reli.
Mwaka 2017, Jimbo la India la Karnataka lilizindua kampeni ya kuwaonya watu kwamba selfie zinaweza kuua baada ya kifo cha wanafunzi wanne. Mwaka huohuo, mtu mmoja alifariki katika eneo la Odisha wakati ndovu ambaye aliuwa akipiga selfie naye alimkamata na kumpiga na chini.