Bondia Mtanzania, Alphonce Mchumiatumbo apigwa KO ya ngumi mbili Urusi
0
October 07, 2019
Bondia namba moja uzito wa juu Tanzania, Alphonce Mchumiatumbo amepigwa na Mrusi, Arstan Yellev kwa Technical Knock Out (TKO) nchini Urusi usiku wa kuamkia leo Jumapili Oktoba 6, 2019.
Katika pambano hilo la raundi 8, Mchumiatumbo alipigwa TKO kunako raundi ya kwanza, Ambapo bondia Arslan Yallyev alimsokomezea masumbwi mawili mazito yaliyompeleka chini Mchumitumbo mara mbili na kujikuta akisalimu amri.
Kocha Mtanzania aliyeambatana na bondia huyo, Anthony Rutha amesema refa alilazimika kumaliza pambano baada ya Mtanzania huyo kupelekwa chini mara mbili mfululizo.
Tags