Bosi Simba Amaliza Utata Wa Kina Mkude


MTENDAJI Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amefunga mjadala wa wachezaji wa kikosi hicho ambao awali ilidaiwa ni watovu wa nidhamu hali iliyofanywa kuwekwa pembeni.



Wachezaji hao ni Jonas Mkude, Clatous Chama, Erasto Nyoni na Gadiel Michael ambapo inaelezwa kuwa, walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Simba ikijiandaa kwenda Kanda ya Ziwa kucheza mechi za Ligi Kuu Bara na wachezaji hao kubaki jijini Dar.


Tangu litokee sakata hilo kumekuwa na maneno mengi yakisemwa kwamba wachezaji hao wamesimamishwa na watakatwa sehemu ya mishahara yao, lakini Mazingisa amesema hamna kitu kama hicho.



“Hakuna mchezaji aliyeadhibiwa bali walisimamishwa kutokana na madai ya utovu wa nidhamu.

“Nilikutana na wachezaji hao na kuzungumza nao mambo yakaisha.



“Niseme tu, hili si kwa wachezaji pekee kwamba ndiyo wanapaswa kuwa na nidhamu bali kwa wote ili kuisaidia Simba kwenda inavyotakiwa ili mambo yaende kwenye mstari,” alisema Mazingisa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad