Chadema Watoa ya Moyoni Kuhusu Mkurugenzi Mpya wa Tume ya Uchaguzi
2
October 01, 2019
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa maoni yake juu ya Mkurugenzi mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt Wilson Charles, na kwamba kwa sasa wamejipanga kushughulika naye kuelekea katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital leo Oktoba 1, 2019, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa chama hicho John Mrema, amesema kwa sasa hawezi kumzungumzia Mkurugenzi aliyepita na badala yake wanamtakia heri na fanaka kwa majukumu yake mengine.
"Aliyepita ameshapita, kwa hiyo hata tukimzungumzia haisaidii, tumtakie kila la heri huko anakoenda kupangiwa kazi nyingine, tushughulike tu na huyu ambaye yupo na tutakayekuwa naye kwenye uchaguzi muda mchache ujao" amesema Mrema.
Mara kwa mara chama hicho kilikuwa kikiingia kwenye migogoro na aliyekuwa Mkurugenzi wa NEC Dkt Athuman Kihamia.
Tags
Wote ni wale wale tu maana ukishateuliwa unakuwa mtu wa kufuata maelekezo ya bosi wako ndiyo maana tunataka tume huru ambayo watendaji wake wanagombea nafasi hizo kwa kupigiwa kura na wananchi na kwenda kuapishwa bungeni na wanaogombea wasiwe makada wa chama chochote hapo tungekuwa na tume huru ya uchaguzi.
ReplyDeleteWewe kwelimdau Shuweini.
DeleteUnafiriuchaguzi niwaKiholela hole..! wa taarifa yako ni kwamba, Vigezo na Masharti yamezingatiwa.
Wewe ishia twita na flashi yako
Sijui umesha ongeza mega byte.?
Ulicho andika ni Utumbo na inaellekea kuwa mpotezaji pesa kwa matumizi yasiyo kuwa lazima.
Au ndiyo mpiga Dili..Vimekaza.
mta jiju awamu yetu.HAPA KAZI TU