Chadema Yajitetea Kutofanya UCHAGUZI...Yasema Kamati Ilibadilisha RATIBA ya Uchaguzi



Kutokana na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kukiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuhusu Uchaguzi, Chama hicho kimesema Katiba ya Chama, Ibara ya 6.3.3 (a) inatoa mamlaka kwa Kamati Kusogeza mbele uchaguzi mkuu wa ndani ya chama

Taarifa yao inaeleza kuwa, Kamati Kuu ya Chama ilikaa kikao Julai 27 na 28, 2019, na kurekebisha ratiba ya uchaguzi ambapo utakamilika mwezi Desemba kwa ngazi ya Taifa

Aidha, chama hicho kimeeleza kuwa katika hatua ya sasa, kinaifanyia kazi barua hiyo ili iweze kuifikia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ndani ya muda husika uliotajwa

Wakati huo huo, kimewahakikishia Viongozi wake, wanachama na Watanzania wote wapenda demokrasia na mabadiliko kuwa hakijakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa nchini wala Katiba ya Chama katika mwenendo wa shughuli zake
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad