Chama tawala Botswana chashinda uchaguzi mkuu
0
October 25, 2019
Chama tawala nchini Botswana cha Democratic Party (BDP) kimeshinda uchaguzi mkuu baada ya kupata viti 29 katika bunge la taifa, ikiwa ni sawa na asilimia 51 ya kura.
Wananchi wa Botswana walipiga kura siku ya Jumatano kulichagua bunge la taifa lenye viti 57 na wawakilishi 490 wa serikali za mitaa, wakati mgombea wa chama kitakachoshinda ndie atakuwa rais.
Mwanasheria Mkuu wa serikali, Terrence Rannowane amesema kuwa licha ya kwamba bado zoezi la kuhesabu kura linaendelea, idadi ya wabunge ilichopata chama cha BDP inamlazimu kumtangaza Mokgweetsi Masisi kuwa rais mteule wa Botswana.
Chama kikuu cha upinzani, Umbrella for Democratic Change, UDC, kimepata viti 13 wakati chama cha Botswana Patriotic Front kimeshinda viti vitatu na chama cha Alliance for Progressive kimepata kiti kimoja, wakati asilimia 73 ya majimbo ya uchaguzi tayari yamekwisha hesabiwa.
Tags