Daktari aliyeisaidia Kumpata Osama Bin Laden Akata Rufaa


Daktari wa PakistanI ambaye aliisaidia Marekani kumpata kiongozi wa kundi la al-Qaeda Osama Bin laden amekata rufaa dhidi ya hukumu yake jela.

Ni mara ya kwanza ambapo kesi ya Shakil Afridi inasikilizwa katika mahakama ya wazi.

Jaji aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 22 mwezi Oktoba kufuatia ombi la waendesha mashtaka.

Kinachodaiwa kufanywa na Daktari Afridi kilikuwa aibu kubwa kwa Pakistani. Lakini yeye mwenyewe anadai ya kwamba alinyimwa haki yake wakati wa kusilikilizwa kwa kesi hiyo ambapo alihukumiwa mika 33 jela.

Hakushtakiwa rasmi kwa jukumu lake katika operesheni hiyo ya mwaka 2011 ya kumsaka na kumuua mtu aliyekuwa akitafutwa sana duniani.

Kufungwa kwake jela kulisababisha hisia kali hatua iliosababisha Marekani kufutilia mbali msaada wake kwa Pakistan wa takriban dola milioni 33 - ikiwa ni dola milioni moja kila mwaka kwa hukumu yake katika mahakama ya Peshawar.

Rais wa Marekani Donald Trump aliahidi katika uchaguzi wa 2016 kwamba atamwachilia huru Afridi baada ya dakika mbili iwapo atachaguliwa - lakini hilo halijafanyika.

Huku daktari huyo akionekana kuwa shujaa Marekani, nchini Pakistani anaonekana kama msaliti ambaye alililetea aibu kwa taifa hilo.

Makomando wa jeshi la wanamaji la Marekani walisafiri kwa helikopta kutoka Afghanistani mpaka Pakistani na kumuua aliyepanga njama za mashambulizi ya Septemba 11 na kuondoka na mwili wake bila kuzuiwa.

Na hatua hiyo ilizua maswali mengi ya iwapo jeshi la Pakistani lilikuwa linajua iwapo Bin Laden alikuwa nchini humo. Pakistani imesalia kuwa mshirika asiyeaminika katika vita vya Marekani dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu.


Dkt Afridi alikuwa daktari mkuu katika hospitali ya wilaya ya Khyber na akiwa mkuu wa huduma za afya alikuwa amesimamia baadhi ya mipango kadhaa ya chanjo zinazofadhiliwa na Marekani.

Kama mfanyakazi wa serikali , alianzisha mpango wa chanjo ya Homa ya Ini (Hepatitis B), ikiwemo katika mji wa Abbottabad ili kubaini iwapo waliokuwa wakiishi katika eneo hilo ni ndugu za bin Laden.


Inadhaniwa kwamba mfanyakazi mmoja wa Dkt Afridi alitembelea nyumba ya akina Osama bin laden na kuchukua vipimo vya damu - lakini haijulikani iwapo hilo lilisaidia Marekani kumpata Osama.

Dkt Afridi alikamatwa mnamo tarehe 23 mwezi Mei 2011 siku chache tu baada ya Bin laden kuuawa. Alidaiwa kuwa na miaka 40 wakati huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad