Dar, Dodoma waongoza ukusanyaji Mapato


Jiji la Dodoma limetajwa kuongoza katika kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 13.0 huku Jiji la Mbeya likiwa la mwisho katika kundi hilo kwa kukusanya Shilingi Bilioni 2.7.

Takwimu hiyo imetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo wakati akitoa taarifa ya mapato ya vyanzo vya ndani vya halmashauri kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka ya mwezi Julai hadi Septemba.

Katika kuzipima halmashauri zote kwa pamoja katika kipindi hiki imeonesha kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekusanya mapato mengi zaidi kuliko halmashauri zote kwa kukusanya Bilioni 13.10 na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ikishika mkia kwa kukusanya Shilingi Milioni 35.15.

Kwa upande wa mapato ya ndani ya halmashauri kimkoa kwa kuzingatia wingi wa mapato, Mhe Jafo amesema Mkoa wa Dar es Salaam ndio ulioongoza kwa kukusanya Shilingi Bilioni 39.5 na Mkoa wa mwisho katika wingi wa ukusanyaji wa mapato ni Mkoa wa Kigoma ambao umekusanya Shilingi Bilioni 2.1 katika kipindi hicho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad