Diamond awapa neno wasanii


Msanii wa muziki, Diamond Platnumz amewataka wasanii wenzake kutumia vivutio vya Taifa katika kazi zao ili kutangaza utalii uliopo nchini.

Diamond Platnumz amesema kwa upande wake yupo tayari kutangaza vivutio mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza nchi.

“Haiwezekani mastaa kutoka nchi zingine kutembelea vivutio vyetu wakati sisi wenyewe tupo karibu na tunashindwa kwenda, mastaa wengi wamekuja nchini kama vile David, Beckham, Lionel Messi wamepanda mlima wetu Kilimanjaro."

“Nimefurahi kupanda Kilimanjaro japokuwa sikufanikiwa kufika kileleni, lakini kwangu ni jambo la kubwa na historia, hivyo wasanii kupitia kazi zetu inabidi tutangaze vivutio vyetu ili watalii waje, nchi ijulikane na tukuze uchumi wetu,” alisema msanii huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad