Dk. Mabodi apokea ujumbe wa watu watano kutoka Chama cha CPC China


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi, ameupokea Ujumbe wa Watu  watano kutoka Chama Cha Kikoministi Cha China (CPC).



Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha (CPC) Mhe.Guo Yezhou wamewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Zanzibar wa Abeid Amani Karume.

Viongozi wengine waliopokea ujumbe huo ni pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar na Watendaji wa ngazi mbali mbali za Chama.

Mara baada ya mapokezi hayo ujumbe huyo uliwasili Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Kisiwandui Zanzibar na kuweka shada la maua katika kaburi  la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.

Lengo la ziara ya ujumbe huo kutoka Jamhuri ya Watu wa China ni kuimarisha mahusiano yaliyodumu kwa miaka mingi baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Kikoministi cha China(CPC).

Aidha,Viongozi hao wa vyama hivyo vyenye undugu wa muda mrefu watazungumzia na kubadilishana uzoefu wa masuala mbali mbali ya Kisiasa, Kiuchumi,Kijamii na uimarishaji wa masuala ya Kidiplomasia.

 Ziara hiyo ya CPC itakuwa ya siku mbili visiwani Zanzibar.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad