DPP Mganga: Hatuoni sababu ya kukataa kupokea fedha za Rugemarila kwa wale wanaorejesha
0
October 04, 2019
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, amesema hawaoni sababu ya kukataa kupokea fedha kwa wale ambao wanataa kurejesha fedha za James Rugemarila.
DPP Mganga aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuwepo kwa baadhi ya mawakili kutaka kufanya utapeli katika mchakato unaoendelea wa washtakiwa wa kesi za uhujumu uchumi ambao wanarejesha fedha.
Akihojiwa kuhusiana na wale ambao wanarejesha fedha walizopewa na Rugemarila alisema wanaotaka kurejesha fedha walizopewa na Rugemarila zinapokelewa na hawaoni sababu ya kuzikataa.
DPP Mganga amesema hawezi kuzuia watu kurejesha na kwamba fedha hizo zitaingia kwenyea akunti maalumu ambayo itatumika kuingiza fedha za washtakiwa wa kesi za uhujumu uchumi.
Alisema kuna akaunti maalum imefunguliwa kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa ajili ya kupokea fedha za mchakato ambao unaendelea.
“Sasa kama mtu anajua alifanya na anaona hawezi kuendelea kuwa na uchafu rohoni unamzuiaje asirejeshe pamoja na kwamba anaona hajafika huko.. lakini anaona haya ni matatizo anaona bora nijisafishe pengine Mungu aendelee kumrehemu vizuri,” alisema
Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmilki mwenza wa zamani wa IPTL yupo gerezani anakabiliwaa na kesi ya uhujumu uchumi.
Mbunge wa Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka juzi amesema uongozi wa shule ya Sekondari ya Barbro Johansson Model utarejesha fedha za msaada walizopokea kutoka kwa mfanyabiashara , James Rugemarila ili aweze kutoka gerezani.
Tibaijuka aliyasema hayo Oktoba 1 mwaka huu kuwa uongozi wa shule hiyo umekaa kikao na kuamua kurejesha fedha hizo walizookea ili kumsaidia mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutoka gerezani.
Tags