Enyi Wanawake Mlioolewa Kuweni Makini sana na Waume Zenu Unapoleta Mdogo Wako wa Kike

Hili jambo ni kuwatahadharisha wanawake ambao wapo ndani ya ndoa na kuwaonya wanaume wote walio ndani ya ndoa waache tabia ya huyu jamaa, pia kutaka ushauri wenu

Kuna binti mmoja tuko kwenye mahusiano kwa mda lengo akimaliza chuo na yakiwa majaliwa ya muumba tufunge ndoa, sasa alipokuja hapa Jijini Dar akawa anaishi kwa dada yake ambaye kuolewa.

Sasa huyo mwanaume amekua akimsumbua sana mpenzi wangu (ambaye ni shemeji yake) kumtaka kimapenzi, hili tatizo limekua likitusumbua akili sana na mpenzi wangu kwa sababu ya kuonyesha msimamo amekua akimtukana bila sababu.

Uzuri ni kwamba sms zote zipo na kila mazungumzo mpenzi wangu anayarecod na mengine yapi kwenye simu yangu ananitumia WhatsApp, yani anavyomtukana wakati mwingine na kumwambia yani unawapa wanaume wengine huko nnje unaninyima mimi.

Uzuri ni kwamba tuko karibu sana na mpenzi wangu kwasababu tunaishi mtaani mmoja kwa hiyo wakati mwingi yupo kwangu akitoka chuo kabla ya kurudi kwao, kwahiyo tumekua tukimrecod huyo baba tukiwa wote bila yeye kujua, na wakati huu sasa hamuheshimu huyo shemeji yake na kujibu anavyotaka na huyo shemeji yake ana umri wa miaka 40-45 na kuendelea.

Cha kusikitisha zaidi amekuja mdogo wake huyo mpenzi wangu aliemaliza secondary yani hata vichichu ndo vimeanza jamaa kaanza kukisumbua nasema kitoto coz ndo kamefikisha 18 juzi, sasa kamelalamika kwa mpenzi wangu kua jamaa anakasumbua balaa.

Sasa wakuu hapa nifanyeje coz huyo mtu kuna siku nahisi kuna siku atambaka kama sio mpenzi wangu basi ni hako kadogo kake, hebu tafakari mkewe yupo na wanaishi wote humo ndani lakini jamaa kakomaa na wadogo zake, huyo baba pamoja mke wake wanajua mimi nina mahusiano na huyo binti.

Ila hawajawahi kuniuliza, tunakaa mtaa mmoja na tinasali kanisa moja, nishaurini nifanyeje coz ushahidi wa record anavyokomaa upo na naweza kuvuruga hata ndoa yao, na pia nawahurimia hawa madogo coz sijui itakuaje na dada yao.

Na nyie wanaume hebu tuachieni hawa wadogo zao tioe acheni tamaa mana hao wadogo zake usipeme, dada yao hata nusu hawafikii.

WANAWAKE KUENI MAKINI NA WAUME ZENU MNAPOWALETA WADOGO ZENU WAZURI KULIKO NYIE KUISHI NA NYIE, sio wote nimeleta tahadhari
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ..binti pamoja na we mchumba. acheni ujinga, kama kweli binti hajafurahia anachofanyiwa na shemeji yake dawa ni kumwambia dada yake na si kubaki mnakusanya ushahidi ili siku akibakwa ndiyo mtoe. Hii tahadhari "WANAWAKE KUENI MAKINI NA WAUME ZENU MNAPOWALETA WADOGO ZENU WAZURI KULIKO NYIE KUISHI NA NYIE" itamaanisha kama mwanamke ataelezwa ukweli na mdogo wake. Dawa ya jipu ni PWAA. Kingine acheni uongo eti ni kitoto kidogo, kinafuata nini kwako, tofauti yako na shemeji ni kwamba yeye kaoa dada mtu, lakini kama kutembea na kitoto kidogo ni kosa basi na wewe mchumba unamakosa. ..NI MAONI YANGU TU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utakuwa unatembeaga na vitoto wewe inavyoonyesha huna hata uchungu mtu wa miaka 18 wewe unaweza kumuona mkubwa kweli angekuwa mtoto wako je au dada yako ungeruhusu acha zako wewe msaidie mtu sio kumponda mtu.

      Delete
  2. Mmh Amesema Ni mdogo wa mpnz wakee amerudi kutoka shule..mi Ushauri wangu Ni vyema mkamwambia Huyo dada coz hata ndoa ikivunjika ivunjike kabla tukio halijatokea...itasaidia kdgo mwanaume hafai Jaman kwann mfuge maovu ya kijinga ningekuwa mimi Huyo binti hata wewe mpenzi wangu usingejua ningepasua jipu bila wasi wasiwasi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad