FIFAYapitisha Panga TFF Yawaondia Vigogo 10


FIFA imepitisha panga ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kula vichwa 10 ambavyo vilikuwa vinaunda Kamati ya Utendaji kwa kutaka vipungue.



Fifa wameitaka TFF kupunguza wajumbe wa kamati hiyo ambayo walikuwa 23 na kuwataka kubakia 13 pekee ikiwa ni mabadiliko ya katiba ya shirikisho hilo pia wakitakiwa kupunguza wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho hilo.



Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao ameliambia Spoti Xtra, kuwa Fifa wamewapa maelekezo ya kutakiwa kupunguza watu hao kwa ajili ya kuendana na mabadiliko ya katiba ya shirikisho hilo na wanasubiri muongozo rasmi.



“Fifa wametoa maelekezo kuwa wajumbe wa kamati ya utendaji wapunguzwe kutoka 23 waliopo sasa hadi kufikia 13 kwa ajili ya kuendana na mabadiliko ya katiba.



“Lakini pia kunatakiwa kupunguzwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF  ambapo mkutano huo utafanyika Desemba, mwaka huu, pia mkutano huo kwa sasa unatakiwa kufanyika mara kila baada ya miezi miwili tofauti na mitatu ilivyokuwa awali,” alisema Kidao.



Katika hatua nyingine Kidao ameweka wazi juu ya TFF kumpa shavu aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura kuwa bosi wa Idara ya Habari na Masoko baada ya kumaliza muda wake katika Bodi ya Ligi.



“Hivi sasa tunatangaza kuwa nafasi yake ipo wazi, hivyo tutaendelea na mchakato wa kumtafuta mtu wa vigezo stahiki aje kuchukua nafasi yake, na hii ni nafasi ya ajira kwa yeyote mwenye sifa ya kutuma maombi basi afanye hivyo,” alisema Kidao.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad