Gwajima : Magufuli sio 'Bookkeeper

 
Ikiwa leo ni siku ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima, amemtakia heri na kumuambia kuwa aendelee na kasi ile ile ya utendaji wake wa kazi, kwani kila kitu kikubwa huanzia


Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Oktoba 29, 2019, Askofu Gwajima amesema kuwa Rais Magufuli, amekuwa ni kiongozi wa mfano hii ni kutokana na utendaji wake wa kazi ambao si lazima mtu auelezee kwa maneno bali ni ule unaoonekana kwa macho.

"Namkumbusha tu mambo makubwa huanza kwa mambo madogo, mtu aliyetoka kijijini kwenye familia za watu wa kawaida, anaweza kuzaliwa na kukua na kuwa mtu wa kuligeuza Taifa letu na hii ndio maana Yesu alizaliwa kwenye holi la Ng'ombe, hakuzaliwa Hospitali, lakini amepewa jina lipitalo majina yote kwahiyo namtakia Mh Rais maisha marefu na 'inspiration' zake kwa nchi andelee nazo ili tufike mahali tunapotakiwa" amesema Akofu Gwajima.

Aidha Gwajima ameongeza kuwa, "Uongozi wake kwanza ni kiongozi 'by performance' na sio kiongozi wa 'bookkeeper' kama viongozi wengine, utendaji wake wa kazi unaelezea kwani ameweza kubadilisha vitu vingi".

Siku kama ya leo ya Oktoba 29, 1959, miaka 60 iliyopita, alizaliwa Rais Dkt John Pombe Magufuli, Kijijini kwao Chato mkoani Geita.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad