Hakimu ‘Akwama’ Kesi ya Kabendera

KESI ya Uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera, imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na Hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo mahakamani.



Kesi hiyo imetajwa na kuahirishwa mahakamani hapo mbele Hakimu Mkazi Vick Mwaikambo. Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mwaikambo, kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.



Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 7, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya sh Milioni 173.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad