DAR ES SAAAM: Staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ anaendelea kung’ara kila kona na sasa amepiga bao lingine la kimataifa.
Harmonize au Harmo, wiki hii ameng’ara tena baada ya kutajwa kama mwanamuziki pekee kutoka Afrika Mashariki atakayewania tuzo kubwa za muziki barani Ulaya za MTV Europe Music Awards kwa mwaka 2019.
Mwaka 2019 vipengele vya Tuzo za MTV Europe Music Awards vimetangazwa na zitafanyika Novemba 3, 2019 jijini London nchini Uingereza ambapo Harmo anashindanishwa na wanamuziki kutoka Afrika Magharibi.
Mbali na Harmo, wanamuziki wengine wanaowania tuzo hiyo kwenye Kipengele cha Best African Act 2019 ni Burna Boy, Teni, Nasty C, Prince Kaybee na Toofan.
Akizungumzia ishu hiyo, meneja wa Harmo; Beauty Mmary ‘Mjerumani’ alisema ni nafasi nyingine kwa mwanamuziki huyo kung’aa kimataifa na kuwaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti kwa kumpigia kura kwa wingi ili alete ushindi Bongo.
“Ni jambo kubwa, tunaomba mashabiki na watu wote wanaopenda muziki huu ufike mbali, basi waendelee kumpa sapoti Harmonize ili tuzo ije Tanzania kwani ni heshima kubwa,” alisema Mjerumani