Majina Ya Wanafunzi Waliopata Mkopo 2019/20 awamu ya kwanza. ....Tazama HAPA
0
October 18, 2019
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa Mwaka wa Kwanza kwa mwaka wa masomo 2019/2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya TZS 113.5 bilioni.
Katika mwaka huu wa masomo, Serikali imetenga TZS 450 bilioni zinazolenga kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 128,285. Kati yao, zaidi ya wanafunzi 45,000 ni wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wenye mikopo wanaoendelea na masomo. Mwaka 2018/2019, fedha zilizotengwa na kutolewa zilikua TZS 427.5 bilioni na ziliwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,283 wakiwemo 41,285 wa mwaka wa kwanza.
Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi, Oktoba 17, 2019) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema katika orodha hiyo, wanaume ni 19,632 (64%) na wanawake ni 11,043 (36%).
==>>KUONA ORODHA YA MAJINA AWAMU YA KWANZA, BOFYA HAPA.
Tags