Hizi Hapa Faida za Bamia Katika Mwili Wako

Hizi Hapa Faida za Bamia Katika Mwili Wako
Bamia ni mboga ya mda kidogo,ilianza kutumika miaka 3500 iliyopita, pia ilikuwa ikijulikana kama lady's finger, mboga hii ina utajiri wa virutubisho mbalimbali ambavyo vina uwezo wa kuboresha afya yako kwa ujumla.Watu walitumia mbegu za bamia badala ya kahawa katika vita kuu ya pili ya dunia

Hivi ni virutubisho vilivyomo kwenye Bamia
Bamia ina madini ya chuma na calcium,na pia ina vitamini A na C. Mboga hii pia ina
thiamine, riboflavin, mafuta na wanga. Zinaweza kutumika zikiwa mbichi au unaweza ukazipika.Kikombe kimoja cha bamia mbichi kina gramu 33 za calories wakati  iliyopikwa ni 25gms. Bamia mbichi ina kiwango kikubwa cha fiber(3.2gms) na iliyopikwa ni 2gramu.
Vilevile bamia mbichi ina wingi wa vitamini A kuliko iliyopikwa. Kuna gramu 21 za vitamini C katika bamia mbichi.

Faida katika Afya yako ukitumia Bamia
Wanasayansi wengi wamethibitisha matumizi ya bamia yana manufaa makubwa katika afya ya Binadamu, baadhi ni pamoja na,

1.Bamia ina kiwango kikubwa cha fiber kinachosaidia kuweka usahihi kiwango cha sukari katika damu
2.Utomvu wa bamia unasaidia kuzuia choresterol na asidi zenye sumu

3.Ina saidia kwa wenye matatizo ya kuvimbiwa

4.Njia ya utumbo mdogo ina aina mbili za bacteria, bacteria wazuri na wabaya, bamia inachochea
kuongezeka kwa bacteria wazuri na kudidimiza ukuaji wa bacteria wabaya

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad