IAAF yaja na sheria mpya ya wanariadha wenye jinsia mbili


Wanariadha wanawake wenye jinsia mbili sasa watalazimika kushusha nusu ya viwango vyao vya homoni za kiume chini ya sheria mpya iliyotolewa na IAAF, sheria ambayo itawahusu wanariadha wenye homoni nyingi za kiume kama Caster Semenya.

Chini ya sheria mpya halali iliyotangazwa wiki hii, wanariadha wenye jinsia mbili hawatakiwi tena kutambuliwa na sheria kwa jinsia zao bali watahitajika kutoa tamko lililosainiwa, la kujitambua kuwa ni wanawake.

Baraza la Shirikisho la Riadha Duniani, lililokutana Doha, limepitisha sheria hiyo inayotaka kupunguza homoni za kiume kwa wanariadha wanawake na kuwa chini ya nanomoles tano kwa lita hali ambayo inapaswa kuendelea kwa kipindi cha angalau miezi 12 kabla ya kutangazwa kuwa wanastahili kushindana kwenye kipengele cha wanawake. Kiwango cha awali kilikuwa ni nanomoles10.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad