Jacob Zuma kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya rushwa


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya rushwa baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake la kutaka kesi hiyo isitishwe kabisa.

Uamuzi huo wa leo una maana kuwa kutakuwa na uchunguzi zaidi kuhusu mpango wa ununuzi wa silaha wa mwaka wa 1999 ambao Zuma anatuhumiwa kwa kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya kutengeneza silaha ya Ufaransa Thales.

Tuhuma hizo ziliibuliwa zaidi ya muongo mmoja uliopita lakini zikaondolewa, na kurejeshwa tena baada ya Ofisi ya Mashitaka kutangaza kuwa kuna ushahidi wa kutosha wa kumfikisha Zuma kizimbani.

Alikuwa rais kutoka mwaka wa 2009 hadi 2018, wakati alipolazimishwa kujiuzulu na chama tawala cha African National Congress ANC kutokana na madai mengine tofauti ya rushwa. Zuma anaweza kukata rufaa uamuzi huo wa leo wa mahakama.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad