Japan kutoungana na Marekani kulinda meli za mafuta

Serikali ya Japan imesema imeamua kutoungana na muungano wa kijeshi wa Marekani katika kulinda meli za mizigo katika eneo la Mashariki ya Kati, badala yake inajipanga kutuma jeshi lake kwa lengo la kuhakikisha usafirishaji salama wa mafuta yanayoingizwa Japan.

Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Japan Yoshihide Suga amesema hata hivyo Japan itafanikisha ushirikiano wa karibu na serikali ya Marekani hata kama haijajiunga na jitihada hiyo, ambayo Marekani inasema ina lengo la kuzilinda meli za mafuta kutokana na kile kinachodaiwa mashambilizi ya Iran.

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amekuwa akijaribu kusaidia kupunguza mvutano kati ya Marekani na Iran.

Ushirikiano wa mataifa hayo mawili umezidi kuzorota tangu mwaka uliopita baada ya Rais Donald Trump kujiondoa katika mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu na kuanzisha upya uwekaji wa vikwazo ambavyo vimezorotesha uchumi wa Iran.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad