Je, Rekodi ya Kipchoge inatambulika Duniani?
0
October 13, 2019
Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge, amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za Marathon duniani, kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya dakika mbili.
Kipchoge ametumia saa 1 na dakika 59 na sekunde 40, kukamilisha rekodi hiyo katika mashindano ya 'Ineos Challenge' mjini Vienna nchini Austria yaliyofanyika leo Jumamosi, Oktoba 12, 2019.
Chakushangaza ni kwamba licha ya Kipchoge kuvunja rekodi hiyo, lakini haitaingia kwenye rekodi ya dunia ya shirikisho la Riadha (IAAF) kutokana na sheria, muundo na taratibu zilizoongoza mbio hizo.
Sababu kubwa nyingine ya kutotambulika kuwa rekodi mpya ya dunia ni kutokana na mashindano hayo kutohusisha watu wote, badala yake kulikuwa na makundi ya wanariadha ambao walikuwa wanamsindikiza kwa kuingia na kutoka kwenye mbio.
Hata hivyo sio mara ya kwanza kwa Bingwa huyo wa Olimpiki kutaka kuweka rekodi hiyo, ambapo mwaka 2017, alichelewa sekunde 25 pekee kuweka rekodi ambayo leo ameiweka.
Tags