Je Wajua Faida za Kutokuvaa Chupi?

Je Wajua Faida za Kutokuvaa Chupi?Leo naomba nikukumbushe somo la Afya ya uzazi. Somo hili litafafanua faida na hasara au madhara yatokanayo na uvaaji wa nguo za ndani hasa Chupi. Uvaaji wa chupi kihistoria ulianza karne ya 19 baada ya uvumbuzi wa viwanda na mapinduzi yake yaliyoambatana na mapinduzi ya teknolojia.

Enzi za mama zetu na babu zetu uvaaji wa chupi haukuwepo hapa Tanzania. Uvaaji wa chupi uliletwa na wamisionari na wakoloni wakati wanaleta dini Africa. Kabla ya hapo waafrica hatukuwa na utamaduni wa KUVAA chupi.

Mtoto akizaliwa hakuvalishwa chupi kamwe kama ilivyo Leo. Mwanamke pia enzi hizo alikuwa havai chupi. Mwanaume naye pia alikuwa havai chupi? Watu wote walikuwa hawavai chupi. Mwanamke alikuwa hachuchumai chini pindi akijisaidia kutokana na kwamba hawakuwa wanavaa chupi hivyo wakitaka kujisaidia haja ndogo walikuwa wanasimama tu na kupanua miguu na kuanza kukojoa.

Nyakati za leo ambapo uvaaji chupi kwa wanaume na wanawake uko juu sana kuanzia watu tunapokuwa watoto wadogo hali ya Afya ya viungo vya uzazi imeendelea kuwa mbaya sana. Yafuatayo ni baadhi ya madhara ya kuvaa chupi :

1. Magonjwa ya "Urinary tract infection" au UTI hayataisha kwako.
Hii hasa ni kwa wanawake wanavaa nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa muda mrefu zaidi ya saa kumi. Unavaa chupi, lakini tight, suruali ya jinzi, nk halafu unashinda na hizo nguo kuanzia asubuhi unapoenda kazini hadi saa mbili usiku unaporudi home. Hiyo ni hatari sana.

Mwanamke anayefanya kazi zinazompasa kuwepo kazini zaidi ya masaa 8 namshauri asiwe anavaa chupi kabisa. Chupi ivaliwe nyakati za hedhi tu. Kama hauko kwenye siku zako vaa suruali tu bila chupi. Au vaa underskirt pekee yake kwa ndani na ndoo uvae nguo yako ya kawaida. Hii itakuepusha na kuugua UTI. Ukiacha sababu za ngono UTI husababishwa na bacteria wanaopendelea mahali penye unyevu na joto. Kwa hiyo mwanamke akivaa nguo nyingi bacteria hao hujipatia joto la kutosha kuzaana.
Mwanamke ni vyema ukaepuka kuvaa nguo za kubana mwili sana ili kuepukana na uwezekano wa kupafanya ukeni pawe na joto sana na ikitokea bacteria mmoja tu akaingia humo atazaa haraka sana na kujikuta UTI inakuwa rafiki yako. Vaa sketi bila chupi au kama kuvaa suruali ni lazima hakikisha unavaa suruali peke yake. Jizoeze tu utazoea. Na ukizoea kuvaa nguo bila chupi utainjoi sana.

2. Magonjwa ya kuvu au fungus hayatakoma kwako.
Bado niko kwa wanawake, kama nilivyoeleza mwanzo hapo magonjwa ya fungus yanasababishwa pia na kuvaa chupi kwa muda mrefu. Chupi inayovaliwa kwa zaidi ya saa 8 lazima italeta ukungu au uvundo sehemu nyeti. Huo uvundo waweza kuleta fungus ukeni. Fungus za ukeni hazina tofauti na zile za miguuni kwa wanaume wanaovaa viatu kwa muda mrefu bila usafi miguuni wa kutosha.

Chupi inakuwa kama socks za wanaume. Mwanamke avaae chupi muda mrefu bila kuruhusu upepo upite ndani ni watapata fungus ukeni sawa na mwanaume anayevaa socksi zisizofaa kiafya. Chupi au socks zinazofaa ni zile za pamba au cotton.

Of course sababu za kupata ugonjwa wa fungus kwa mwanamke siyo tu kuvaa chupi inayobanaaaa kwa muda mrefu ni pamoja na kutawadha kwa kutumia maji.

Wanawake wengi hawajui kutawadha kwa kutumia maji. Wengi wamalizapo kujitawadha haja kubwa ndipo hurudi kujisafisha ukeni. Hii ni hatari sana kwani bacteria watokanao na kinyesi unawahamisha kutoka nyuma na kuwaleta mbele.

Mwanamke unapaswa kutawadha kwanza mbele kisha umalizie nyuma.

Yaani hakikisha kuwa uchafu wa nyuma unaoweza kuwa umebakia kwenye vidole vyako usiuingize ukeni kwa namna yoyote. Tawadha pande zote lakini uhakikishe kuwa haviingiliani mbele na nyuma. Sawa dada yangu? Uko poa hapo?

Kikubwa hapa ni usafi wa mbele na nyuma. Usafi wa chupi zetu. Uvaaji chupi wetu.

Kwa mfano uwapo safarini tena safari ndefu ya zaidi ya saa 8 ni vyema ukasafiri bila kuvaa chupi isipokuwa tu kama uko kwenye siku zile za adabu. Hata kama uko kwenye siku za adabu ni vyema ukasafiri bila kuvaa manguo mengi sana yanayobana mwili. Vaa chupi na sketi au suruali isiyoubana sana mwili wako.


3. Chupi husababisha ugumba kwa wanaume.
Sababu nyingi za ugumba tunaweza ukizipata kutoka kwa madaktari wetu wa hospitali zetu. Lakini ukija kwangu mimi Daktari wa magonjwa ya tabia (Lifestyle Based Diseases Doctor) nitakuongezea sababu nyingine ya ugumba wa wanaume kuwa ni kuvaa chupi zinazobana sana.

Mwanaume shujaa havai chupi. Anavaa kaptura badala ya chupi. Tena havai kaptura inayobana sana. Anavaa isiyobana viungo muhimu kwa uzalishaji wa watoto. Mbegu za kiume huzalishwa kwa wingi wakati wa baridi. Kuvaa chupi inayobana kwa muda mrefu husababisha pumbu kuchemka sana na kushindwa kuzalisha mbegu nyingi. Mwanaume mwenye mbegu chache hushindwa kutungisha mimba kwani mbegu zake zinakwenda ukeni kwa uchache na kushindwa kuogelea ukeni.


4. Chupi husababisha miwasho sana kwenye mapaja ya mwanaume na mwanamke.
Epuka kuvaa chupi zinazobana ili kuepukana na miwasho.

5. Chupi husababisha michubuko ya mapaja.
Ukivaa chupi kwa muda mrefu utajikuta umepata michubuko mapajani karibu na uume au uke .

6. Uvaaji chupi usiku huchelewesha tendo la ndoa.
Mwanaume anapohitaji vitu adimu usiku wakatimwingine anapaswa kujichotea tu kirahisi kwani ni mke wake halali lakini akikutana na chupi inakuwa kikwazo. Mwanamke usilale na chupi usiku. Unaogopa nini? Hakuna majambazi wala moto. Nani alikwambia ulale na chupi eti unajihami na ajali za moto usiku.? Mbona tangu umelala na chupi usiku hakuna ajali ya moto iliyokwishatokea.

Acheni kuvaa chupi enyi wanawake ili ikitokea waume zenu tunahitaji naniii usiku tujipatie kwa wepesi! Au Siyo?

Tangu niache kuvaa chupi sijawahi tena kuwashwa mapajani wala mke wangu hajawa na taarifa za fungus na UTI kama zamani alipokea hajalielewa somo hili. Na wewe pia nakushauri uache kuvaa chupi kuanzia leo Uwe na afya bora maeneo yote nyeti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad