JPM Aamsha Balaa kwa Mkurugenzi Nachingwea

 RAIS John  Magufuli ameendelea na ziara yake mkoani Lindi ambapo leo Jumatano, Oktoba 16, 2019, amefika katika Wilaya ya Nachingwea na kuwaahidi wananchi wa mkoa huo kwamba vijiji ambavyo havijapata umeme chini ya mradi wa REA, vitapata.



“Ndugu zangu wa Nachingwea ndio maana nipo hapa leo, nawashukuru kwa kunipa kura. Nachingwea imebadilika sana si kama zamani. Tunafahamu kama umeme haujafika katika maeneo yote ya Nachingwea, mwanzo ni mgumu. Vile vijiji vyote ambavyo havijapata umeme chini ya mradi wa REA vitapata, nchi inabadilika naomba muamini.



“Mkurugenzi umesema mnapokea Tsh bilioni 27 kwa ajili ya halmashauri ya hapa Nachingwea, hizo fedha mnapeleka wapi na mmesema soko hili mnalikarabati kwa mapato yenu ya ndani.



“Nawashukuru ndugu zangu wa Nachingwea kwa kuwa wakweli, ukweli humweka mtu huru, Tsh milioni 71 zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa soko lakini mambo yanasuasua. Hayo mengine niachieni mimi nitafanya maamuzi.



“Nafahamu shida mnayopitia barabara, ndiyo maana nimekuja na usafiri wa gari, ningeweza kuja na ‘helikopta’ lakini nimeamua kutumia barabara ili niyapate maumivu mnayoyapitia. Nataka niwahakikishie kuwa hii barabara ya kilometa 45 ya Nachingwea tutaijenga katika kiwango cha lami.



“Tunawaomba ‘Makangomba’ muache ukangomba tunataka zao la korosho liwafaidishe wakulima wenyewe,” amesema Magufuli.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad