JPM Amchana Live Nape Nnauye Mbele ya Wanamtama "Ulifanya Dhambi Zako Sasa Nikakusamehe"


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Magufuli amesema kuwa amemsamehe kwa moyo wote Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.



Rais Magufuli amesema hayo akiwa Mtama na kuwaomba wananchi hao, Wampe mbunge huyo ushirikiano wa kutosha ili kuijenga Mtama.

“Najua wananchi wako wanakupenda, Na mimi nakupenda. Ulifanya dhambi zako nikakusamehe. Nape nimeshamsamehe sio mtuhumiwa hana dhambi yoyote naomba mshirikiane nae kuijenga Mtama. ” Rais Magufuli.

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye mwezi uliopita alikutana na Rais Magufuli Ikulu kwa lengo la kuomba msamaha, Baada ya sauti yake kuvuja mitandaoni akimteta Rais.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli ametangaza kuwa Halmashauri ya Lindi Vijijini ibadilishwe na iitwe Mtama.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad