JPM Awaka: Wanaume wa Rukwa Msiwape Mimba Watoto


Rais Dk. John Magufuli, leo Oktoba 7, 2019 amezindua Mradi wa Huduma za Maji Safi na Usafi wa Mazingira uliopo Majengo, Sumbawanga uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (KFW) na Umoja wa Ulaya (EU), chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Sumbawanga (SUWASA).



Pia, Rais amezungumza katika mkutano wa hadhara, Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Hii ni mwendelezo wa ziara yake ya mkoa wa Rukwa.



“Mkoa wa Rukwa una idadi kubwa ya mimba za utotoni. Kwa mwaka 2018 pekee wanafunzi 229 walipewa ujauzito, hii ni hasara kubwa kwa Serikali inayogharamia elimu na kwa wananchi walipa kodi. Wazazi acheni kuoza watoto wakiwa wadogo, mkiona ameota matiti mnasema amekomaa, hapana, wanaume wa Rukwa waacheni watoto wasome.



“Tumeshasambaza umeme katika vijiji 7400 umeme kutoka vijiji 2000, Tunataka tuhakikishe kabla ya 2022 kupitia mradi wa REA(III) karibu vijiji vyote vya Tanzania vipate umeme.



“Tumetenga Tsh bilioni 55.2, tutajenga Uwanja wa Ndege mkubwa mkoani Rukwa, utahudumia hadi watu wa Tunduma, DRC, mpaka Zambia wote watakuja hapa, itakuwa kituo cha usafiri kwenye ukanda huu.”



“Ukishatoboa na ukapata maji kuyasambaza sio tatizo ni sawa na mtu kupata mke kuzaa mtoto sio kazi tena, ndugu zetu wa Ulaya hawa wameshatupa maji, nimemuelekeza Waziri aanze kuyasambaza maji. Kuna wakati fulani Mainjinia wangu niliwatuma wakalala kwenye Makalavati na walipoamka saa 4 asubuhi wakajikuta wako nje, hii ndiyo Rukwa.



“Wizara ya Fedha muandike, muombe pesa kwa ajili ya Rukwa pekee, tutaangalia na wizara ambazo zimezubaa kutumia hela, tutaleta fedha hizo hapa Rukwa kwa ajili ya miradi ya maji.”



“Kuna malalamiko Mamba anakula watu, Mamba na Viboko wanaishi ziwani na kwenye mabwawa, ninyi mmewafuata, Viboko na Mamba tunawahutaji, pia wananchi tunawahitaji, kwa hiyo lazima mgawane, msiende sana kwenye maeneo yao.



“Niwaibie siri, kuna gesi ya Helium imegunduliwa hapa katika Bonde la Rukwa, ni gesi nypesi yenye matumizi makubwa sana. Ningekuwa najua Kifipa ningewaambia, lakini naamini mtaelewa tu. Mungu ameibariki mno Rukwa,” amesema Magufuli.



JPM: Mlichanga shilingi ngapi kwa ajili ya soko la Nelson Mandela?

Mwenyekiti wa Soko: Soko letu liliungua, tumekusanya Tsh 15m wanataka kujenga ghorofa.

Meya: Mhe. Rais tumeshafanya maandiko, tunataka kujenga soko la kisasa…. Tulitaka tuwarudishie wakakataa.

JPM: RC mjifunze kumaliza matatizo, tangu 2016 hadi leo mnajenga ghorofa la kuuzia nyanya? Waacheni wauze kwenye soko lao, nitachangia Tsh 200m waliboreshe.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad