JPM "Ningetaka Utajiri Ningekua Bilionea"
0
October 11, 2019
Rais Dkt John Magufuli amesema, angetaka utajiri angekua bilionea lakini kazi yake kubwa ni kuhakikisha nchi inanyooka.
Akizungumza na wananchi wa Mpanda Mkoani Katavi jana Oktoba 10 wakati akilihutubia Taifa, Rais Magufuli amnesema amekuwa waziri kwa miaka 20, angekuwa na shida na utajiri angekuwa bilionea, lakini kazi aliyoimba ni moja tu, kunyoosha nchi ambapo amemewanyoosha mafisadi.
“Nimewanyoosha Mafisadi, walituchezea mno, walituibia mno. Wamedhulumu rasilimali za Watanzania. Ninanchotaka tu kuwaomba ndugu zangu chapeni kazi, mengine mtuachie serikali, nataka miaka inayokuja mtu awe anatoka hapa anakula breakfast hapa, lunch anakwenda kula Tabora, dinner anakula hapa jioni,” Alisema
Mbali na hilo, Rais Magufuli ametoa maagizo kwa Ofisa Elimu wa Mkoa wa Katavi, asipange walimu mjini tu, wapange na vijijini na asiyetaka kwenda kijijini aache kazi na kuongeza kuwa hata madaktari, manesi na watumishi wengine wapangwe vijijini.
Tags